Matatizo mengi yanayotufanya tuugue yanaweza kuzuilika. Baadhi ya njia za kuzuia magonjwa huhitaji muda, juhudi na fedha zaidi mwanzoni, lakini hunusuru muda na fedha baadae kwa kutuepeusha na magonjwa. Sura hii inaelezea jinsi ya kuzuia kuharisha na magonjwa mengine yanayosababishwa na vijidudu vilivyomo kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama. Matatizo mengi yanayoathiri tumbo na matumbo yanaweza kuepukwa kwa kunawa mikono, kuzingatia usafi katika kuandaa na kuhifadhi chakula, kutumia vyoo kwa usahihi, na kunywa maji safi na salama. Ili kujifunza jinsi ya kuzuia: utapiamlo, kisukari, ugonjwa wa moyo, na matatizo mengine yanayosababishwa na lishe duni, angalia Lishe bora hutengeneza afya bora. nimonia au kichomi,kifua kikuu, na matatizo mengine ya kupumua angalia Matatizo katika kupumua na kikohozi (kinaandaliwa). matatizo ya kiafya yanayosababishwa na utupaji hovyo wa taka za kawaida na taka zingine, angalia Taka za kawaida, taka za hospitalini na uchafuzi wa mazingira (ki