Wanaojisaidia kwenye chupa wabanwe


Image result for mkojo kwenye chupa

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, amesema viongozi wa masoko, mitaa na maeneo ya kazi hasa masoko wanapaswa kusimamia sheria ili kudhibiti wanaochafua mazingira kwa kujisaidia katika chupa za maji na kuzirusha katika makazi au maeneo wazi.
DC Kisare alisema hayo hivi karibuni baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliosema baadhi ya wafanyabiashara katika Soko la Simu 2000 lililopo Ubungo Dar es Salaam, wanajisaidia haja ndogo katika chupa kisha kuzirusha katika mitalo na maeneo mengine ya wazi yakiwamo makazi ya watu na barabarani.
Mkuu wa Wilaya alisema bila wafanyabiashara hao kutambua umuhimu wa usafi, kutunza mazingira na uongozi wa soko kuchukua hatua makini, ipo hatari ya kuibuka magonjwa ya mlipuko ukiwamo ugonjwa wa kipindupindu.
“Viongozi wa masoko na maeneo wana wajibu wa kusimamia usafi na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokwenda kinyume maana kusambaza uchafu kama huo ni kosa la jinai kwa sababu mtu anayefanya hivyo anasababisha usumbufu, kero na kuhatarisha afya na maisha ya watu,” alisema DC Kisare.
Rukia Wandwi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni alisema, “Hali hiyo inasababisha kero na inaweza kuhatarisha afya na maisha ya watu maana baadhi ya wamachinga pale, wanajisaidia katika chupa za maji kisha wanazirusha katika uzio. Sasa unakuta asubuhi watu tunafanya kazi ya kuokota chupa hizo zilizowekwa choo.
IFIKE WAKATI TUWE WASTAARAB KWA AJILI YA AFYA ZETU NA MAENDELEO YA TAIFA LETU, HUU SI UUNGWANA HATA KIDOGO.

Comments

Popular posts from this blog

Nchi 10 zenye mazingira safi duniani.

Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo Tanzania

Maji na usafi wa Mazingira