Posts

Showing posts from September, 2017

Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo Tanzania

Nuzulack Dausen September 13, 2017 MWANANCHI: Mwanza/Dar. Magonjwa ya malaria, maradhi yanayoathiri mfumo wa kupumua, Ukimwi, upungufu wa damu na magonjwa ya moyo ni miongoni mwa magonjwa yaliyochangia kwa kiwango kikubwa kuchukua uhai wa Watanzania 247,976 kwa miaka 10 iliyopita katika hospitali mbalimbali hapa nchini, utafiti waonyesha. Katika ufunguzi wa warsha kuhusu sababu za vifo katika hospitali nchini iliyofanyika jijini Mwanza juzi, Mtafiti Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Leonard Mboera alisema lengo la utafiti huo ni kutambua ongezeko la maradhi yanayoathiri jamii. Dk Mboera alisema vifo hivyo vilitolewa taarifa kwa kipindi cha miaka 10 kati ya 2006 na 2015, huku vifo vingi vikiathiri wanaume kuliko wanawake. Alisema katika kundi la watoto chini ya miaka mitano vilichangia asilimia 20 ya vifo vyote. Utafiti Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mercy Chiduo akimuonyesha Mganga