Waziri azindua kampeni ya matumizi ya vyoo



By Reginald Miruko, Mwananchi
Dodoma. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo amezindua kampeni mpya ya kitaifa ya usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo mjini Dodoma iliyobatizwa “Nipo Tayari”
Kampeni hiyo imekuja baada ya ile ya kwanza iliyoanza mwaka 2012 hadi Juni 2016 ambayo amesema ilifanikisha kuongeza uelewa katika masuala ya usafi wa mazingira.
Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na kunakuwa na matumizi ya vyoo bora kuanzia ngazi ya kaya, taasisi na maeneo ya umma.
#NIPO TAYARI WEWE JE?, CHUKUA HATUA SASA.

Comments

Popular posts from this blog

Nchi 10 zenye mazingira safi duniani.

Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo Tanzania

Maji na usafi wa Mazingira