Kunawa mikono, Kinga imara dhidi ya magonjwa ya tumbo na kuhara
Sababu kuu za vifo vya watoto
Shirika la afya (WHO) duniani
linakadiria kwamba magonjwa ya kuhara na maambukizi ya mfumo wa upumuaji
yanahusika kwa theruthi mbili ya vifo vya watoto (tazama kielelezo no 1). Shirika
la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linakadiria kwamba ugonjwa wa
kuhara peke yake huua mtoto mmoja kila baada ya sekunde30. Vifo ving vya watoto
hutokea kw a watu maskini Zaidi katika nchi zeneye kipato cha kati au chini. Kwamaana
hiyo Tanzania ni moja wapo kati ya nchi amabazo hupoteza watoto 2880 kwa siku na watoto 1,051,200 kwa mwaka, hii ni idadi kubwa
kwa taifa.
Tanzania ni moja wapo kati ya nchi
amabazo hupoteza watoto 2880 kwa
siku na watoto 1,051,200 kwa mwaka,
hii ni idadi kubwa kwa taifa.
Kielelezo
no.1 Chanzo: Shirika la Afya Duniani 2001
TUNAWEZA KUZUIA UGONJWA WA KUHARA?
Najua utakuwa umeshtushwa kwa kiasi kikubwa jinsi
ugonjwa wa kuhara unavyolitafuna taifa letu. Swali ni je tunaweza kuzuia ugonjwa wa kuhara?
Jibu ni Ndio. Ugonjwa wa kuhara unazuilika
na kuepukika kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kabla hatujaangalia ni namna gani
tunaweza kuepuka ugonjwa wa kuhara ni lazima kwanza tuangalie ugonjwa huu
unasababishwa na nini?
Vinyesi vya binadamu ni chanzo kikuu cha vijidudu
visababishavyo magonjwa ya kuhara.
Vilevile ni vyanzo vya maambukizi ya shingela,
homa ya matumbo, kipindupindu,
pamoja na maambukizi mengine yote ya magonjwa ya tumbo na baadhi ya maambukizi
ya mfumo wa upumuaji.
Inaaminika kwamba gramu moja ya kinyesi inaweza kuwa
na viruisi milioni 10 na bakteria milioni 1. Vijidudu husafirishwa kutoka kwa
mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama ilivyooneshwa katika kielelezo no. 2 hapo
chini pia magonjwa ya kuhara na tumbo yanasambazwa kwa kiasi kikubwa na nzi,
hivo watu hushauriwa kuweka mazingira salama ya vyoo, sehemu ya kupikia chakula
na kufunika vyakula ili kuzuia inzi kuyafikia maeneo hayo.
Kielelezo
no. 2. Chanzo. Hesperian Health Guide
Najua ulikuwa na shauku kubwa ya kujua ni namna gani
unaweza kujilinda mwenyewe, familia yako na jamii kwa ujumla juu ya magonjwa ya
kuhara. Hizi hapa ni njia muhimu za kuepuka na kuzuia magonjwa ya kuhara:
1. Kunawa
mikono vizuri baada ya:
Kabla ya Kula
Kuwashika wanyama kama mbwa, paka, mbuzi,
ngombe, nguruwe, kuku n.k
Kutoka chooni
2. Kuosha
matunda kabla ya kula
3. Kuepuka
kula vyakula vilivyo chacha au ambavyo havijapashwa
4. Kuepuka
kunywa maji ambayo hayajatibiwa au kuchemshwa.
5. Kufunika
vyakula vizuri baada ya kupikwa.
Utafiti wa hivi karibuni (Curtis na Cairncross, 2003) unaonesha
kunawa mikono vizuri kwa sabuni baada ya kugusa kinyesi (baada ya haja kubwa na
baada ya kuzoa kinyesi cha motto) kunaweza kupunguza maambukizo ya ugonjwa wa
kuhara kwa asilimia 41-47.
Hivyo sabuni inaondoa kila aina ya uchafu na kuua
vijidudu viliyo katika mikono.
Natumaini utakuwa umejifunza na
utaifundisha jamii juu ya ugojwa wa kuhara, unaweza kushea na wengine katika
mitandao ya kijamii. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeisaidia Tanzania.
Comments
Post a Comment