Maji na usafi wa Mazingira

Matatizo mengi yanayotufanya tuugue yanaweza kuzuilika. Baadhi ya njia za kuzuia magonjwa huhitaji muda, juhudi na fedha zaidi mwanzoni, lakini hunusuru muda na fedha baadae kwa kutuepeusha na magonjwa.

Sura hii inaelezea jinsi ya kuzuia kuharisha na magonjwa mengine yanayosababishwa na vijidudu vilivyomo kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama. Matatizo mengi yanayoathiri tumbo na matumbo yanaweza kuepukwa kwa kunawa mikono, kuzingatia usafi katika kuandaa na kuhifadhi chakula, kutumia vyoo kwa usahihi, na kunywa maji safi na salama.

 Ili kujifunza jinsi ya kuzuia:

  •  utapiamlo, kisukari, ugonjwa wa moyo, na matatizo mengine yanayosababishwa na lishe duni, angalia Lishe bora hutengeneza afya bora.
  • nimonia au kichomi,kifua kikuu, na matatizo mengine ya kupumua angalia Matatizo katika kupumua na kikohozi (kinaandaliwa). 
  • matatizo ya kiafya yanayosababishwa na utupaji hovyo wa taka za kawaida na taka zingine, angalia Taka za kawaida, taka za hospitalini na uchafuzi wa mazingira (kinaandaliwa).
  •  malaria, homa ya denge, na magonjwa mengine yanayoambukizwa kupitia mbu, angalia Baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukizwa (kinaandaliwa). Jinsi ugonjwa wa kuharisha unavyoenea Vijidudu na minyoo hueneza ugonjwa wa kuharisha kwa kusafiri njia zifuatazo kutoka kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama:
Jinsi ugonjwa wa kuharisha unavyoenea:
Vijidudu na minyoo hueneza ugonjwa wa kuharisha kwa kusafiri njia zifuatazo kutoka kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama:


                                   Img source: Hesperian Health Guide

Vijidudu vya magonjwa pia husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa kuwa wanafamilia huishi pamoja, vijidudu na magonjwa yanaweza kuenea kwa urahisi kwa familia nzima.


1. Mvua kubwa zinaweza kusababisha mfereji wazi wa maji machafu kutoka chooni
kufurika. Mbwa anayepita mitaani kwenye maji hayo anaweza kubeba kinyesi kwenye miguu yake.

2. Mbwa anaweza kuingia ndani ya nyumba, mtoto kucheza naye na kujipaka           kinyesi kwenye mikono yake.

3. Baadaye mtoto analia na mama yake kumbembeleza. Mtoto anakamata sketi         ya mama yake na kuichafua na kinyesi.


4. Mama mwenye majukumu mengi anaanza kuandaa chakula cha jioni. Anatumia sketi yake iliyochafuliwa kukinga mikono yake isiungue wakati wa kuepua chakula.


5. Familia inakula na baada ya muda mfupi kila mtu anaanza kuharisha.

Comments

Popular posts from this blog

Nchi 10 zenye mazingira safi duniani.

Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo Tanzania